Mikutano ya kisheria husaidia kutatua migogoro ya wananchi
12 January 2022, 7:01 pm
Na,Rosemary Bundala
Mikutano ya kisheria katika halmashauri za vijiji imetajwa kuwa njia mojawapo ya kutatua matatizo pamoja na migogoro kwa wananchi
Hayo yamezungumzwa na wanachi wa wilaya ya uvinza mkoani Kigoma Bwana VICENT LAZARO na Bi MWAMINI JUMA wakati wakizungumza na redio uvinza fm ambapo wamesema mikutano ya kisheria husaidia pale panapokuwa na migogoro na matatizo ya kijiji
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kibaoni wilayani uvinza bwana MUSSA RAMADHANI amesema mikutano ya kijiji husaidia japo mwitikio hua mdogo kutoka kwa wananchi na akatoa ushauri kwa kwa wananchi katika kuhakikisha wanajitokeza kushiriki katika mikutano ya kijiji
Nae mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha ruchugi wilayani uvinza mkoani kigoma bwana RAMADHANI SAID KAYUNGILO ameelezea maana ya mikutano ya kisheria pamoja na umuhimu wa mikutano hiyo
Mikutano ya kisheria katika ngazi za vijiji bado inaonekana kuwa chanzo bora cha wananchi kusemea matatizo na shida za kijiji kwa urahisi katika maeneo yote nchini.