Radi yaua watu watano wa familia tofauti
5 January 2022, 5:44 pm
Na,Editha Edward
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Kigoma zikiambatana na radi imepelekea ajali ya radi ambapo imepiga watu watano na kusababisha vifo
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma JAMES MANYAMA amesema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 04/01/2022 majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha kibuye kata ya kumsenga tarafa ya mabamba wilaya ya kibondo
Kamanda MANYAMA amesema Watoto wote wanne walikuwa wakicheza chini ya mti wa muembe kisha kupigwa na radi na kufariki papo hapo
Aidha kamanda MANYAMA amesema miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo na ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma hasa katika kipindi hiki cha mvua