Mabomba ya maji yenye thamani ya shilingi milioni 600 yatolewa na serikali
24/11/2021, 3:59 pm
Na,Glory Paschal
Mabomba ya Maji yenye thamani ya Shilingi milioni 600 yametolewa na Serikali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambayo yanaanza kutandikwa katika kata kadhaa ikiwemo kata ya Bangwe
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. ESTER MAHAWE amesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya kutimiza adhima ya kumtua ndoo Mama kichwani ifikapo mwaka 2025 kwa kuhakikisha huduma ya maji inafika maeneo yote
Naye Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira KUWASA, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhandisi JONAS MBIKE, amesema wamejipanga kuhakikisha wanafikisha huduma ya maji kwa wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hiyo, huku akitaja maeneo ambayo mabomba hayo yatatandikwa
Baadhi ya wananchi Kata ya Bangwe, ambao ni miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na utandikaji wa mabomba hayo, wameiomba KUWASA kuanza zoezi hilo mapema, ili waondokane na adhaa inayowakabili ya kutopata maji safi na salama.