Taa za kuongozea magari zenye thamani ya milioni 55 zazinduliwa
8 October 2021, 6:08 pm
Na,Glory Paschal
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma THOBIAS ANDENGENYE amezindua taa za kuongozea magari na watumiaji wengine wa barabara za njia nne katika barabara ya Lumumba Mjini Kigoma ambazo thamani yake ni Shilingi Milioni 55
Akizungumza mara baada ya kuzindua taa hizo, Kamishina wa Polisi Thobias Andengenye amewataka wananchi kuheshimu matumizi ya barabara
Kwa upande wake Meneja wa TANROAD Mkoani Kigoma Eng NARCIS CHOMA amesema mradi huo ni mwendelezo wa maagizo ya serikali ya kuboresho ya miundombinu ya barabara huku akieleza mikakati ya TANROAD kwa miaka ijayo
Baadhi ya viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma ESTHER MAHAWE, na Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini wamewataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya barabara
Hata hivyo baadhi ya madereva wa vyombo vya moto pamoja na watembea kwa miguu wamelitaka jeshi la polisi kutoa elimu kwenye maeneo yote yenye taa hizo kwa angalau majuma mawili.