Uvinza FM

Wananchi wajengewa daraja ili kuepukana na vifo vilivyokuwa vikitokea

28 September 2021, 7:12 pm

Na,Glory Paschal

Wananchi wa Kata za Bitale na Mkongoro Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma wameondokana na adha ya kusombwa na Maji ya Mto Nyabigufa na kusababisha vifo pamoja na  kupoteza mali zao, baada ya Serikali kujenga daraja la Kisasa la Mawe.

Wamesema kupatikana kwa daraja katika mto huo wanaona kama ndoto ambayo ilisubiriwa kwa muda mrefu bila matumaini na sasa wanaamini vifo vilivyokuwa vinatokea na kupoteza mali zao kwa kusombwa na maji imekwisha ikiwa ni baada ya kupatikana daraja la kisasa.

Sauti za wananchi wa kata ya bitale

Kiongozi wa Mbio za mwenge Luteni Josephine Mwambashi amezindua rasmi daraja hilo la nyabigufa na kuahidi kutatua tatizo la ukosefu wa kituo cha afya huku mkuu wa wilaya ya Kigoma ESTER MAHAWE akiagiza kutunzwa kwa miundombinu ya daraja hilo.

 Miradi nane yenye thamani ya zaidi ya Bilioni Moja imepitiwa na Mwenge wa uhuru kwa wilaya ya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma  ambapo imewekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa.