Waziri mkuu amewahakikishia wakulima wa mazao ya kimkakati masoko
16/09/2021, 9:10 pm
Na,Glory Paschal
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Mjaliwa Kassim amewahakikishia wakulima wanaolima mazao ya kimakakati nchini kuwawezesha katika mchakato wa kuandaa kulima na kuwatafutia masoko ya ndani na nje ya nchi.
Ametoa kauli hiyo alipotembelea Shamba la michikichi katika kambi ya JKT Burombola iliyopo wilayani Kigoma na kusisitiza kuwa mazao yote tisa ya kimakakati nchini yapo chini ya uangalizi wa serikali kuhakikisha yanaleta tija kwa uchumi wa nchi na mkulima mmoja mmoja.
Amesema serikali imeamua kuongeza Mazao ya kimakakati kufikia tisa lengo ni kuongeza tija katika mazao ya kibiashara yatakayoiwezesha nchi kimapato na kutimiza hilo wakulima watasimamiwa katika maeneo yao ili kuhakikisha uzalishaji wake unakidhi mahitaji ya soko.
Mkuu wa Kambi ya JKT Burombola Iliyopo Wilayani Kigoma mkoani hapa amesema tayari hekari 500 zimeshaandaliwa na kupandwa lengo likiwa ni kufikia hekali 2000.