UNDP kuwafunda wabunifu mbalimbali mkoani Kigoma
13/09/2021, 3:40 pm
Na,Glory Paschal
Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Maendeleo UNDP, likishirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo sido mkoani kigoma wametoa mafunzo kwa wabunifu wanaoanza ili kuibua bunifu na kuahindanisha kazi zao ambapo mshindi wa kwanza atapatazawadi ya milioni 10
Meneja wa Sido Mkoa wa Kigoma Bw. GERVAS NTAHAMBA amesema katika mkoa wa Kigoma kuna bunifu nyingi sana lakini bado jitihada za kuwafikia wabunifu hao imekuwa ni changamoto na kueleza kuwa shindano hilo litasaidia kuwafikia wabunifu wengi walikuwa hawafikiwi na kuweza kuwaibua
Kwa Upande wake Afisa Miradi Kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Maendeleo UNDP, Bw. DEOGRATIAS MTEMBELA amesema wameendesha zoezi la kuwagundua wasajiliamali wabunifu kwenye maeneo ya ufugaji, Kilimo na makundi mengine ili kutatua changamoto zinazoyakabili makundi mbalimbali hasa wanawake na vijana
Baadhi ya wabunifu hao waliopatiwa mafunzo hayo akiwemo Bi. VAILETH VICTOR wamesema elimu walioipata wanaamini itawasaidia kuendelea kuwa wabunifu wazuri zaidi katika masuala ya maendeleo huku wakiomba serikali na wadau kuendelea kuwaibua watu wengine ambao hawajaweza kuonekana ili kuonyesha ujuzi walio nao
Mafunzi hayo ya Ubunifu yanatarajia kufikia tamati September 14 Mwaka huu ambapo washindi wa shindano la ubunifu watatangazwa washindi watano na kuwawezesha zawadi ambazo zitawasaidia kujiendeleza kama wabunifu.