Ugumu wa maisha huwapelekea waendesha bajaji kubeba zaidi ya abiria watatu
6 September 2021, 4:31 pm
Na,Mwanaid Suleiman
Baadhi ya waendesha bajaji wilayani uvinza mkoani kigoma wamesema kuwa ugumu wa maisha hupelekea kubeba abiria zaidi ya watatu kwenye bajaji licha ya kwenda kinyume na sheria za barabaarani
Hayo yamebainishwa na bw ALLY MOHAMED pamoja na ATHUMANI AHMED ambao wamesema kuwa huwa wanabeba abiria zaidi ya watatu ili kukidhi mahitaji yao
Akizungumza na redio uvinza fm mwenyekiti wa waendesha bajaji wilayani uvinza Bw.HALIS JUMA HALIS amekiri kuwepo kwa baadhi ya waendesha bajaji kubeba abiria wengi ikiwa ni kinyume na utaratibu wa sheria za barabarni
Aidha mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya uvinza SHABAN JUMA ameeleza mikakati thabiti ili kutokomeza uvunjaji wa sheria
Hata hivyo kutokana na sheria za barabarani bajaji inatakiwa kubeba abiria wasiopungua watu watatu.