Apoteza maisha kwa kukatwa na kitu kikali shingoni
2 September 2021, 5:51 pm
Na,Jacob Kapaya
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JACKIAS KIPARA mkazi wa kijiji cha Ruchugi wilayani Uvinza mkoani Kigoma mwenye umri wa miaka 31 amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kigoma JAMES MANYAMA amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na hapa analizungumzia
Katika hatua nyingine kamanda MANYAMA amewashukuru wananchi na kuwahimiza kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa
Mwenyekiti wa kijiji cha Ruchugi Ramadhan Said amekiri kupokea taarifa ya kifo hicho huku akiweka wazi aina ya matukio ambayo yamewahi kujitokeza ndani ya kijiji hicho.
Redio uvinza FM imepata nafasi ya kuzungumza na ndugu wa karibu wa marehemu ambae ni LUCAS KIPARA amesema kuwa mpaka kifo kinamkuta kijana huyo hakuwa katika mazingira ya Nyumbani.
Ikumbukwe kuwa marehemu ameacha mke pamoja na watoto 5 ambapo kati ya hao watoto wawili wanasoma shule darasa la kwanza na watoto 3 hawajaanza shule