Wanafunzi wa kike waiomba serikali kuwaletea walimu wa kike mashuleni ili kutatuliwa changamoto zao
25 August 2021, 5:56 pm
Na,Christina Daud
Baadhi ya Wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari nguruka wilayani uvinza mkoani kigoma wanapata changamoto ya kuwa na walimu wa kike wa kutosha mashuleni kwa ajili ya kueleza shida zao hususani suala la hedhi wanapokua shuleni
Wakizungumza na redio uvinza fm wamesema wakiingia katika mzunguko huo kuna wengine wanashindwa kuendelea na vipindi vya darasani kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo kuogopa kuwaambia walimu wa kiume pindi wanapokuwa katika hali hiyo .
Nae mwalimu matroni wa shule hiyo GLADSY WALUHIGA amesema wanafunzi wa kike wanatakiwa kuwa huru wasiwe waoga katika kuwaelezea walimu wa kiume matatizo yao kwani nao pia ni waelewa.
Aidha watoto wa kike ambao tayari wameshaingia katika hali ya kupata hedhi hawatakiwi kuwa waoga kuzungumza na wazazi wao pamoja na walimu wa kiume pindi wanapokuwa katika hali hiyo.