Wazazi na walezi washauriwa kutowaruhusu watoto kusafirishwa
19 August 2021, 4:23 pm
Na,Glory Paschal
Wazazi na Walezi Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wameshauriwa kutoruhusu watoto wao kusafirishwa kwenda kutumikishwa katika shughuli mbalimbali kinyume cha sheria
Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya Kakonko Bw. Mohamed Shauri amesema baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakishawishika na kuwaruhusu watoto wao kwenda kutumikishwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi
Hata hivyo redio uvinza imefanikiwa kuzungumza na mzazi ambaye aliruhusu mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 14 kwenda kutumikishwa katika kazi za ndani Huko Jijini Dar es Salaam ambapo amesema ni mwaka wa tatu sasa hana mawasiliano na mwanaye wala hajui mtoto huyo anaishije
Nao baadhi ya wananchi wa wilaya za kakonko na kibondo wameitaka Serikali kuwachukulia hatua za kisheria madalali wanaobainika kuwasafirisha watoto hao
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kakonko, Kanali Evance Mesha Masala amesema idadi ya watoto wanaosafirishwa kwenda Mwanza ni kubwa licha ya kuwa ni kinyume cha sheria na kwamba viongozi na jamii wanapaswa kudhibiti vitendo hivyo.