Wananchi walia na ukosefu wa maji
12/08/2021, 4:31 pm
Na,Mwanaid Suleiman
Wakazi wa kijiji cha Ruchugi Wilayani Uvinza mkoani Kigoma wameiomba serikali kutataua changamoto ya maji inayowakumba katika kijiji hicho hasa katika kipindi cha kiangazi
Hayo yamesemwa na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ruchugi kuwa changamoto hiyo imekua kero kwa muda mrefu huku wakihitaji serikali iwasaidie kusambaza mabomba kwa wingi na kuepusha kufuata maji kwa umbali mrefu
Akizungumza na redio Uvinza fm mwenyekiti wa kijiji cha Ruchugi bw Ramadhan Saidi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa wana mikakakati thabiti ili kuweza kuondoa changamoto hiyo
Aidha mwenyekiti wa bodi ya maji wilayani uvinza bw sayaredi nyamtongo amesema kuwa wana mpango wa kujenga tanki la maji ambalo litakua limerahisisha upatikanaji wa maji katika kijiji hicho
Hata hivyo Maji katika kijiji cha ruchugi imekua changamoto kubwa hali inayopelekea kununua dumu la maji la lita 20 kwa sh 500 hasa katika msimu huu wa kiangazi