Corona yaathiri Wafanyabiashara wa samaki na dagaa
5 July 2021, 5:55 pm
Na,Glory Paschal
Baadhi ya Wavuvi na Wafanyabiashara wa Samaki na Dagaa Mkoani Kigoma Wamesema Kufungwa kwa Mipaka ya Nchi Jirani Kutokana na Maambukizi ya Ugonjwa wa Corona Kumeathiri Biashara zao
Wavuvi Pamoja na Wafanyabiashara ambao Wamesema hali ya biashara imekuwa Ngumu Kutokana na Idadi Kubwa Ya Wafanyabiashara Kutoka Nje ya Nchi Waliokuwa Wakifika Katika Mialo ya Dagaa Na Samaki Mkoani Kigoma Kushindwa Kuingia Kutokana na Mipaka yao Kufungwa.
Wamesema iwapo Serikali itasaidia Kuzishawishi Nchi Hizo Kulegeza Masharti kwa Wafanyabiashara Wanaoingia na Kutoka Katika Nchi Hizo itasaidia kupunguza changamoto hizo.
Afisa Biashara Mkoa wa Kigoma Deogratius Sangu licha Ya Kukiri Kuwepo Kwa Changamoto za Kibiashara Baada Ya Kufungwa kwa Mipaka Lakini Ameshauri Wavuvi na Wafanyabiashara Kuheshimu Taratibu Zilizowekwa Katika Kukabiliana na Ugonjwa Huo.