Wananchi Waomba Muongozo Chanjo ya Corona
05/07/2021, 5:43 pm
Na,Glory Paschal
Wananchi wilayani kasulu mkoani kigoma wameiomba serikali kuharakisha kutoa muongozo wa chanjo ya virusi vya corona ili waweze kupata elimu zaidi kuhusu chanjo hiyo ya virusi vya corona ambayo wamekuwa wakiisikia kutoka nchi jirani
Wamesema hayo Wakati Wakizungumza na Redio Uvinza fm, ilipotembelea Mjini humo ambapo wamesema kumekuwa na propaganda nyingi kutoka kwa baadhi ya watu juu ya chanjo ya virusi vya corona hali inayowapa hofu katika kupata chanjo hiyo
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya kasulu Dr. Peter Njanga amesema kuwa hadi sasa miongozo juu ya chanjo itakayotumika hapa nchini haijatoka hivyo kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zilizotolewa mpaka hapo wizara ya afya itapotoa miongozo kuhusu chanjo ya virusi vya covid19
Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya afya maendeleo ya jamii Prof. Abel Makubi amesema kuwa tayari kuna muongozo maalumu ambao unaandaliwa na serikali katika kusimamia Chanjo na utakapokuwa tayari utawekwa wazi kwa kila mwananchi