Jeshi la polisi latakiwa kufanya kazi zao kwa weledi
24/06/2021, 7:31 pm
Na,Glory Paschal
Watendaji wa Jeshi la polisi pamoja na mahakama Mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi ili kutokomeza mimba za utotoni
Hayo yameelezwa na Katibu Tawala Mkoani hapa Rashid Kassim Mchatta katika mkutano wa utetezi kuhusu haki za watoto ulioandaliwa na Shirika la We World kuangazia mimba za utotoni na madhara yake Mkoani hapa
Amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakitengeneza mianya ya rushwa kwa watuhumiwa na kupelekea kesi nyingi kufutwa
Kwa upande wake Afisa maendeleo Mkoani Kigoma Msafiri Nzunuri amesema endapo jamii itashirikiana vyema tatizo hili la mimba za utotoni litafikia ukomo mkoani hapa
Nae Mchungaji Justin Sologo kutoka Umoja wa Makanisa Mkoani Kigoma amesema mimba pamoja na ndoa za utotoni zitatokomezwa pale tu jamii itakapofuata taratibu zilizowekwa na Serikali kuhusu umri sahihi wa kuolewa na kubeba ujauzito kwa wanawake
Aidha jamii ikishirikiana kwa pamoja ina uwezo wa kutokomeza mimba za utotoni, na kwa mwaka 2020 Mkoa wa Kigoma ulikuwa na asilimia 20 ya mimba za utotoni na kati ya hizo wanafunzi 25 wa shule za msingi hawakufanya mtihani wa kuhitimu kutokana na kuwa wajawazito