Michango katika shule za msingi na sekondari ni hiari
7 June 2021, 5:14 pm
Na,Mwanaid Suleiman
Serikali imesema uchangiaji wa michango katika shule za msingi na sekondari ni wa hiari na hauusishwi kwa wanafunzi kuzuia masomo yao ikiwa hajalipa michango hiyo
Hayo yamejiri leo bungeni jijini Dodoma wakati Naibu waziri wa TAMISEMI mh David Silinde alipokua akijibu swali la mbunge wa Nkasi kaskazini Haida Joseph Kenani lililohoji kwanini wazazi wanachangishwa michango ya kuchangia elimu kwa shule ya msingi na sekondari wakati serikali imesema elimu ni bure
Hata hivyo waziri wa elimu sayansi na teknologia professa Joyce Ndalichako ameongezea kwa kutoa wito kwa wazazi kuendelea kutoa ushirikiano na serikali ili watoto waweze kupata elimu bora
Aidha mh David silinde amehitimisha kwa kusema serikali inatakiwa kufanya tathimini upya ili kuboresha sera ya elimu na elimu kwa ujumla.