Mradi wa maji kakonko wafikia asilimia 65
1 June 2021, 4:26 pm
Na,Rosemary Bundala
Serikali imesema hadi kufikia disemba 2020 tayari miradi kumi na tano ilikuwa inatekelezwa katika wilaya ya kakonko ambapo miradi kumi na nne imekamilika na inatoa huduma ya maji kwa wananchi na mradi mmoja uliobaki ni mradi wa kakonko ambao utekelezwaji wake umefikia asilimia 65 na unatarajia kuhudumia mji wa kakonko pamoja na kijiji cha kasuga
Hayo yamejiri leo bungeni jijini Dodoma wakati Naibu waziri wa maji mhandisi Maryprisca Mahundi alipokuwa akijibu swali la mbunge wa buyungu mh Aloyce john kamamba lililohoj ni kwanini miradi ya maji ya kakonko haijakamilika kwa muda mrefu na lini mji huo na vitongoji vyake utapata majisafi na salama na ya kutosha
Naibu maji 01Aidha mh mahundi amesema kuwa mradi wa maji wa kakonko unatekelezwa na Ruwasa kwa kutumia wataalamu wake wa ndani kwa ajili ya kuukamilisha mradi huo ambapo mchakato huo unafanyika kwa awamu
Katika hatua nyingine mh Mahundi amesema katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 serikali pia imepanga kujenga miradi mipya katika vijiji vya chilambo na kokinonko ,ukarabati na utanuzi wa mradi wa muhange kwenda muhangejuu na shule ya sekondari ndalichako pamoja na kuchimba visima virefu katika vijiji viwili vya chilambo na nyakiobe
Bunge limeendelea leo jijini Dodoma ambapo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki Liberata Mulamula anatarajiwa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na wabunge watapata nafasi ya kujadili kile ambacho kitakuwa kimewasilishwa.