Serikali kuendelea kutatua migogoro ya ardhi
28 May 2021, 7:29 pm
Na,Mwanaid Suleiman
Serikali imesema inaendelea kutatua migogoro ya ardhi ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu
Hayo yamejiri leo bungeni jijini Dodoma wakati naibu waziri wa ardhi nyumba maendeleo na makazi mh Angelina mabula alipokua akijibu swali la mbunge wa viti maalum mh jackline kaicha Andrew lililohoji ni lini serikali itamaliza migogoro ya ardhi katika mikoa ya Tabora na Singida
Hatahivyo mh Angelina mabula ametoa rai kwa taasisi za umma ambazo hazilipi fidia kwa wananchi zikiwa zinachangia kwa asilimia 39 migogoro ya ardhi hapa nchini
Aidha kwa mwaka wa fedha 2020/21 wizara ya ardhi iliagiza ofisi zote za i mikoa kuanzisha majedwali ya migogogo ya ardhi ili kuibanisha na kuitambua .