Serikali kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo
26 May 2021, 7:28 pm
Na,Rosemary Bundala
Serikali imesema imenza kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo kwa maana ya mbolea mbegu na viwatilifu ,kuratibu mahitaji ya pembejeo kutoka katika mikoa na kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya makampuni kupeleka na kuuza
Hayo yamejiri leo bungeni Jijini Dodoma wakati naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Bi. Stela Simon Fiayo lililohoji je ni lini serikali italeta pembejeo za kilimo zenye bei nafuu ili wananchi waweze kuzimudu
Aidha naibu Bashe amesema kuwa mikakati mingine ni kuanzisha mifumo ya uhalamiaji wa sekta hasa ikiwemo uanzishwaji wa mfuko wa pembejeo(credit quarantee scheme) pia kufuta na kupunguza baadhi ya tozo na ada kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita serikalli imepitia na kufuta tozo kumi na mbili katika mbegu na tozo nne za mbolea ili kupunguza bei na gharama za pembejeo hizo
Hata hivyo Naibu waziri Bashe Amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mikakati ya upatikanaji wa pembejeo kwa kuvutia wawekezaji wa makampuni binafsi hasa katika eneo la mbegu na mikataba maalumu kwa ajili ya kupunguza gharama
Bunge limeendelea leo Jijini Dodoma ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa fedha 2021/22 ambayo ni kiasi cha Shilingi bilioni 294.1.