Ukosefu wa maji wawaliza wananchi
20 May 2021, 7:27 pm
Na,Editha Edward
Wananchi wa kijiji cha Ruchugi wilayani uvinza mkoani kigoma wameiomba serikali iwatengenezee magati ya maji waliyoyaweka ili maji yaweze kutoka na kuondokana na adha wanayopata ya kutembea umbali mrefu kufuata maji
Wakizungumza na redio uvinza fm wananchi wa kijiji hicho RUKMAN , HILDA ,NA NEEMA wamesema changamoto ya maji imekuwa ni kero kwani maji wanayanunua kwa dumu moja shilingi miambili hamsini hadi miatatu
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho bw.RAMADHAN KAYUNGIRO amesema jambo hilo wameshaliongea kwenye kikao chao cha ndani hivyo amewaomba wananchi wa kijiji hicho wawe na subira ili maji yaweze kupatikana
Aidha bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania lilipitisha bajeti ya maji nchi nzima zaidi ya bilioni miasita.