Uvinza FM

Magoti yatumika kama Madawati Shuleni

18 May 2021, 8:12 pm

Na,Timotheo Leonardi

Wanafunzi  katika shule ya Msingi shikizi kutoka shule mama ya Muungano iliyopo kijiji cha Ruchugi Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma hawana madawati haliinayopelekea kukaa kwenye benchi  nahatimaye kupata ugumu wakati wakiandika masomo yao

Pichani ni wanafunzi

Hayo wameyasema wakati Radio Uvinza fm ilipofika katika shule hiyo kujionea halihalisi nakusema kuwa serikali hainabudi kuwatazama kwa jicho la tatu kuwaondolea changamoto hiyo

Sauti za Wanafunzi

Baadhi ya walimu wa kujitolea katika shule hiyo wamesema ukosefu wa madawati ni changamoto kubwa nakwamba serikali hainabudi kuiboresha shule hiyo kwakutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa madawati

Sauti za Walimu

Kwa upandewake Diwani wa kata ya Uvinza BI: Aloka Mashaka amesema kuwa serikali inaweka mikakati yakuhakikisha inawarekebishia madawati kwa kushirikiana na nguvu za wananchi

Sauti ya Diwani

Aidha shule ya msingi shikizi ya Kazaroho inajumla ya wanafunzi 238 wote wakiwa hawana madawati haliambayo husababisha  mwanafunzi kutoandika vizuri