Wafanyabiashara walia na ulinzi
18/05/2021, 7:33 pm
Na,Mwanaid Suleiman
Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Uvinza Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wamesema wanashindwa kuongeza bidhaa katika maduka yao kutokana na kuhofia usalama uliopo katika eneo hilo
Hayo yamebainishwa na JUMA RASHID pamoja na TAMIM JACKSON wakati Redio Uvinza fm ilipofika kutazama namna wafayabiashara wanavyofanyakazi , huku wakisema inawawia vigumu kuongeza bidhaa kutokana nakutokuwepo kwa walinzi wa kutosha
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao bw. JONATHAN MANYAGA amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na amesema kwamba atawaitisha wafanyabiashara wote ili kuwapa elimu yakujua umuhimu wa uwepo wa walinzi katika Soko hilo
Naye mwenyekiti wa kijiji cha uvinza amesema kuwa wanafanya mikakati ya kuweka ulinzi shirikishi ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo mizuri ya ulinzi ili kuepuka vitendo vya kiuhalifu
Aidha kuwepo kwa walinzi katika eneo lolote lile nimoja ya njia zakuwahakikishia Raia ulinzi na usalama wa mali zao.