Uvinza FM

NBC yazindua klabu ya Wafanyabiashara

13 May 2021, 5:28 pm

Benki ya NBC imezindua klabu ya wafanyabiashara wa benki hiyo mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya mipango ya benki hiyo kusogeza huduma kwa wateja wake sambamba na kujenga mtandao ambao utawasaidia  wafanyabiashara  ,na wateja wa benki hiyo kufanya biashara zao kwa tija

Akizungumza katika uzinduzi huo  Mkurugenzi Mtendaji wa benki  hiyo Theobald Sabia amesema lengo kubwa la klabu hiyo ni kuwakutanisha wafanyabiashara  na watoa huduma mbalimbali kwa pamoja kwenye sekta ya biashara ili kufahamu changamoto zinazowakabili na ziweze kutatuliwa

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji NBC

Mkurugenzi huyo amesema  kwa kupitia kwenye klabu za biashara benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyabiashara hao ambao ndiyo msingi mkubwa wa kuwafanya wafanye biashara zao kwa tija ambapo mafunzo yanayotolewa yanazingatia taratibu mbalimbali za kuwafanya wapige hatua za maendeleo kwenye kusimamia biashara

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji NBC

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, bw. Rashid Mchatta akizindua klabu  hiyo yabiashara kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Kamishina wa Jeshi la polisi Thobias Andengenye amesema kuwa mafunzo ya kujenga mtandao kwa wafanyabiashara ndiyo msingi mkubwa utakaowawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa faida

Sauti ya Katibu tawala Kigoma

Nao Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki kwenye  uzinduzi huo  wameeleza faida kubwa ambayo wameipata kwakuhudhuria mafunzo kutokana na mada zilizotolewa kuishi ndani ya wafanyabiasharaambazo zitawafanya kufanya biashara zao kwa faida.