KUWASA wakanusha kuwabambikizia bili za maji wateja
12 May 2021, 4:40 pm
Na,Glory Paschal
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji, KUWASA wamekanusha taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji Ewura kuwa wamekuwa wakiwabambikiza bili za maji wateja
Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bw. Josephati Rwegasila amekiri kuwepo na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu kwa mwaka jana na tayari wameshawachukulia hatua
Amesema ili kuondoa changamoto hiyo tayari mamlaka imeanza kutumia mfumo mpya ambao umeanza mwaka huu tofauti na mfumo wa awali
Naye Kaimu Meneja wa biashara wa Mamlaka ya maji Godfrey Robini amesema mfumo huo mpya umekuwa ukimpa taarifa mteja ili aweze kuhakiki taarifa hizo kabla ya kupatiwa bili
Nao baadhi ya wateja wamesema mfumo huo wa kubambikiwa bili kubwa za maji upo jambo ambalo limekuwa likisababisha wananchi kutumia gharama kubwa kulipia bili hizo