Uvinza FM

Kilomita kumi za lami zawanyima usingizi Wananchi

10 May 2021, 4:35 pm

Na,Timotheo Leonardi

Wananchi wa kijiji cha Uvinza Mkoani Kigoma wameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya kilomita 10 yenye kiwango cha lami iliyoahidiwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho wamesema barabara hiyo hainabudi kujengwa kwani ikikamilika itaondoa adha wanayoipata katika shughuli zao za kila siku

Sauti za wananchi

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Uvinza Bi.Aloka Mashaka amewaondoa wasiwasi wananchi wa kata hiyo kuwa atasimama nao kikamilifu ili waweze kujengewa lami kama walivyo ahidiwa na Rais

Sauti ya Diwani wa Uvinza

Hata hivyo wananchi wote kwa  pamoja wamekubaliana kuendelea kuilinda barabara hiyo ambayo tayari mita miatisa zimekwisha kukamilika, huku wakipendekeza  itapewa jina la Magufuli

Aidha ujenzi wa barabara nzuri kwa kiwango cha lami ni miongoni mwa njia zakurahisisha shughuli za usafirishaji abiria pamoja na kusaidia kukuza uchumi kwa kasi Zaidi.