Wanahabari Wafundwa
26 April 2021, 8:02 pm
Na,Glory Paschal
Waandishi wa Habari wametakiwa kutumia kalamu zao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Ukatili katika kupinga vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vitendo ambavyo vimeshamili kwenye jamii
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Media Insititute of Southern Africa (MISA) Bi. Salome Kitomali wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wanawake kutoka katika mikoa ya Tabora, Katavi, Rukwa na Kigoma ambayo yamefanyika Mkoani hapa
Amesema waandishi wa habari wanapaswa kuendelea kuripoti matukio ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili vinavyoendelea kutokea ili kuhakikisha elimu inawafikia wananchi hasa wanawake na watoto ambao ndio wahanga zaidi
Naye afisa miradi kutoka taasisi ya Misa Tanzania, Bi. Lucy Kilanga amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari wanawake kujiamini katika kuvumbua matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwakandamiza kuanzia kwenye ngazi za maamuzi
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kufahamu namna ya kuandika habari zinazohusu masuala ya unyanyasaji na namna ya kuwatetea wanawake na watoto kwa ujumla.