Ushirikiano hafifu chanzo cha ukatili wakijinsia Mkoani Kigoma
22 April 2021, 5:24 pm
KIGOMA
Na, Glory Kusaga
Jumla ya Kesi 881 za vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia Mkoani Kigoma zimeripotiwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba Mwaka jana hadi Machi 2021 huku kesi 138 tu ndizo zimefika mahakamani huku changamoto ikitajwa kuwa ni ushirikiano hafifu wa jamii kutoa taarifa za vitendo hivyo
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Dawati la Jinsia mkoa wa Kigoma Inspekta Doris William Sweke wakati wa kikao kilichowakutanisha wadau wa masuala ya ukatili Mkoani kigoma ambapo amesema kesi nyingi hazifanikiwi kutokana na jamii kuchelewa kutoa taarifa za watu wanaotekeleza ukatili huo
Naye hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya Kigoma Eva Mushi amesema kesi nyingi zimekuwa zikichelewa kutolewa hukumu kutokana na ucheleweshwaji wa ushahidi kutoka kwa mhanga wa matukio ya ukatili
Kwa upande wake Mgeni rasmi wa Mkutano huo Moses Msuluzya ambaye amemwakilisha Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma amesema ni wajibu wa viongozi kuwa kitu kimoja kushughulikia kesi za ukatili
Nao baadhi ya wadau wa kupinga vitendo vya ukatili Mkoani Kigoma wamesema ukatili umekithiri kutokana ulevi uliopindukia kwa wazazi na walezi