Mafuriko yakumba Kaya 50
18 April 2021, 8:56 am
KIGOMA
Na; Glory Kusaga
Takribani kaya 50 zilizopo Kata ya Katubuka manispaa ya kigoma ujiji Mkoani Kigoma zimekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani kigoma.Baadhi ya waathirika Wamesema changamoto ya maji kukaa katika makazi yao ni kubwa na kuiomba serikali kutuma wataalamu kuwasaidia kutatua changamoto hiyo.
Ni miezi miwili sasa tangu eneo hilo kuanza kujaa maji ambapo kulingana na historia kumekuwa na bwawa ambalo kila mwaka wakati wa mvua maji hujaa lakini kwa mwaka huu hali imezidi kuwa mbaya zaidi kiasi cha kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
wataalamu kutoka manispaa ya Kigoma ujiji wamefika eneo hilo kujionea hali halisi na kuzungumza na waathirika , ikaibuka hoja ya kuwahamisha kutoka eneo hilo baada ya kukosekana namna nyingine bora Zaidi ya kuwasaidia kuepukana na adha hiyo.
Diwani wa kata ya katubuka Moshi Mayengo anaeleza kwasasa hatua iliyochukuliwa kuokoa wakazi waliopata mafuriko hayo ni kuwahamisha kwa majirani huku hatua za ziada zikiendelea kuchukuliwa.