Tumbatu FM

Elimu ya ufugaji nyuki yatolewa Tumbatu

16 March 2026, 3:34 pm

Ni picha ya Katibu Tawala Wilaya Ndogo Tumbatu Khatib Habib Ali (aliyepo katikati ) akiwa katika ufunguzi wa mafunzo ya ufugaji nyuki (Picha na Vuai Juma)

“Miradi mingi imekua ikianzishwa lakini kutokana na utekelezaji usioridhisha imekuwa haileti matunda hivyo nilazima muwe wakwanza kubadilika pia makundi mnayoyaongoza muyafikie na mkae kwa pamoja ili mpangilie vizuri namna ya kutekeleza mradi huu”

Na Vuai Juma.

Kamati za uvuvi na mazingira kisiwani Tumbatu zimetakiwa kutekeleza majukumu yao kwa usashihi ili kuweza kufikia malengo yaliyopelekea kuanzishwa katika jamii.

Wito huo umetolewa na katibu tawala wilaya ndogo Tumbatu Katibu Habib Ali wakati akizindua mafunzo ya siku mbili kuhusu ufugaji wa nyuki yaliyoandaliwa nashirika linaloshuhulika na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi hapa Tanzania  (TCAN) huko afisi ya Wilaya ndogo Tumbatu.

Amesema ili kufikia maendeleo ya kweli na kupata faida katika kazi zao ni lazima wafikishe elimu wanayo patiwa kwa jamii hasa makundi wanayo yawakilisha kwa lengo la kutanua uelewa wa harakati zao.

Hata hivyo amewataka kuitumia vyema elimu waliyo wapitiwa kwenye mafunzo hayo kwani ndio njia sahihi ya kupata ufanisi na kufaidika na mradi huo.

Sauti ya Katibu Tawala Wilaya Ndogo Tumbatu Khatib Habib Ali akiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanakamaati za uvuvi na mazingira Tumbatu.

Kwaupande wake Afisa nyuki kutoka wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar Asia Yusuf  amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha ufugaji wa nyuki unazidi kuenea maeneo yote ya Zanzibar huku Tumbatu ikiwa na upekee kutokana na uwepo wa miti aina ya mikoko ambayo nimuhimu kwa kazi hiyo.

Hata hivyo amewataka washiriki hao Pamoja na wafugaji wa nyuki kwa ujumla kuhakikisha wanasimamia mfumo mzuri wa ufugaji wa nyuki sambamba na kupata masoko ya ndani nanje ya Zanzibar kwaajili ya kuuza asali wanayozalisha.

Ni sauti kutoka kwa afisa nyuki kutoka wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar Asia Yusuf.
Ni picha ya washiriki wa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kutoka shehia tatu za Tumbatu (Picha Na Vuai Juma)  

“Mafunzo haya tumeyapokea kwa mikono miwili tunatambua umuhimu wa kupewa elimu hii tutafanya kila jitihada tuweze kuyatumia vyema kama ilivyokusudiwa hatimae tuweze kunufaika nayo”

Naowa washiriki wa mafunzo hayo wamesema wamefurahishwa sana kwa kupatiwa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kutokana na umuhimu wake mkubwa huku wakiwataka vijana kuzitumia fursa kama hizo zinapojitokeza kwenye harakati zao na kuahidi Kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo kwaajili ya kupajipatia kipato na kujikwamua na umaskini.

Nisauti ya baadhi ya washiriki waliopatiwa elimu kuhusu ufugaji wa nyuki.

Jumla ya Shehia nne zimefikiwa na mradi huo ikiwemo Uvivini pamoja na Gomani na Matakuja,