Tumbatu FM

Kalamu zenu zitumike kuwatetea watu waishio vijijini

13 March 2026, 10:30 am

Picha ya wandishi wa habari wakiwa kwenye kikao cha kuutambulisha mradi unaohusu haki za binadamu na utawala bora unaotekelezwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kilichofanyika welezo mjini Zanzibar (Picha na Vuai Juma)

“Wajibu wenu kwa wananchi ni kuweza kufanya utafiti kwalengo la kugundua changamoto mbali mbali zinazoikumba jamii hasa maeneo ya vijijini ili kuzisema na kupatiwa ufumbuzi”

Na Vuai Juma.

Vyombo vya Habari vimetakiwa kufanya utetezi kwa makundi ya kinamama vijana na watu wenye ulemavu hasa wanaoishi maeneo ya vijijini kuhusu changamoto wanazokumbana nazo ili waweze kupata haki zao.

Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa mradi wa uwezeshaji wa jamii kwa ajili ya haki za binadamu na utawalabora kutoka idara ya jamii kanisa katoliki jimbo la Zanzibar Sister Editha Simwe wakati wa kikao na wandishi wa habari cha kutambulisha mradi huo.

Amesema mradio huo unalenga kuongeza uelewa wa haki za binadamu na maarifa ya kisheria kwa  wanajamii kupitia huduma za msada wa kisheria na utowaji wa vifaa vya kielimu Pamoja na kuboresha  mifumo ya utawala upatikanaji wa elimu jumuishi kwa wasichana na watoto wenye  ulemavu na kuwajengea uwezo walimu kupitia mafunzo maalum ya kitaaluma.

Ni sauti ya 2 kutoka kwa mratibu wa mradi wa uwezeshaji wa jamii Sister Editha Simwe.

Hata hivyo amewataka kuwasaidia wakinamama na wasichana Pamoja na watoto kwenye masuala ya kielimu jambo ambalo litapelekea kuinua kiwango cha elimu kwa makundi hayo sambamba na kuwahimiza kutoa ushirikiano wa pamoja katika kuisaidia jamii hasa kwenye kupinga masuala ya udhalilishaji.

Sauti ya 2 ya Sister Editha Simwe ambaye ni mratibu wa mradi wa uwezeshaji wa jamii.
Hii ni picha ya ndugu Moh’d Khatibu anaefanya kazi ya ushari kwenye mradi wa haki za binadamu na utawala bora unaosimamiwa na Kanisa katolik jimbo la Zanzibar (Picha na Vuai Juma)

Kwa upande wake mshauri elekezi  wa mradi huo Moh’d Khatib amesema wamegundua uwepo wa uelewa mdogo wa masuala ya haki na sheria  kuwepo wa matukio mengi ya udhalilishaji ambayo yamekuwa hayaripotiwi uwepo wa ndoa za mapema  wanawake kutojishuhulisha na masuala ya kiuchumi na atoto wenye ulemavu kusoma kwenye mazingira magumu.

Ni sauti ua mshauri elekezi  Moh’d Khatib akizungumza na wanahabari.

Aidha amewataka wananchi kuanza kuchukua hatua kwa kuacha tabia ya kutoripoti matukio ya udhalilishaji  na kuwaficha watoto wenye ulemavu kwa kuwafungia ndani na kupigania watu wenye mahitaji maalum washirikishwe kwenye masuala ya kutoa maamuzi.

Ni mwendelezo wa sauti ya mshauri elekezi  wa mradi Moh’d Khatib.

Mradi wa uwezeshaji wa haki za binadamu na utawala bora unatekeleza ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo jumla ya shehia tano za wilaya ya Kaskazini “B” ambazo ni Mkataleni Mahonda Kitope Misufini na majenzi zinanufaika na maradi huo.