Tumbatu FM

Watendaji wa shirika la posta Zanzibar wapewa nyenzo

13 February 2026, 6:38 pm

Picha ya Waziri wa Wizara ya mawasiliano technologia habari na ubunifu Zanzibar  Mudrik Ramadhan Soraga ( alievaa kanzu nyeupe na koti) akiwa katika zoezi la kukabidhi vifaa vya kutendea kazi kwa watendaji wa shirika la posta Tanzania tawi la Zanzibar lilopo kijangwani pamoja na masheha. Picha na Juma Haji.

Ikiwa tutaimarisha mfumo wa kutoa vifaa kwa wafanya kazi kila baada ya muda ninjia pekee ya kuimarisha uwajibikaji kwa watendaji”

Na Juma Haji.

Waziri wa Wizara ya mawasiliano teknolojia, habari na ubunifu Zanzibar  Mudrik Ramadhan Soraga amesema azma ya Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na ile ya mapinduzi ya Zanzibar ya kuweka kipaumbele mageuzi ya kidigitali ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akikabidhi vitendetea kazi ikiwemo magari kwa shirika la posta Tanzania Ofisi ya Zanzibar na vishikwambi kwa masheha kwa niaba ya wizara ya mawasiliano teknolojia habari  Tanzania amesema vifaa hivyo vitawawezesha watendaji wa shika kutoa huduma zenye ubora zinazoendana na kasi ya kidigitali duniani .

Amesema hatua hii inakwenda sambamba na utekelezaji wa sera na mikakati ya serikali yakujenga Tanzania ya kidijitali katika kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato kupitia mitandao inayoshimamiwa na shirika hilo.

Sauti ya Mudrik Ramadhan Soraga – Waziri wa Wizara ya mawasiliano technologia habari na ubunifu Zanzibar

Akitoa salam za serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa niaba ya Wizara ya mawasiliano teknolojia ya habari mkurugenzi msaidizi wa anuwani za makazi Tanzania Bi Edtha Turuka amesema Wizara imekusudia kuweka mazingira wezeshi kwa viongozi wa kata mitaa na mashehia ili kila mwananchi awezekutambulika kupitia anuani yake.

Amesema ili kuongeza kasi ya kazi kwa watendaji wa serekali za mitaa Serikali imetoa jumla ya vishikwambi 3482. Vitakavyotumika kukuhanyia taarifa za wananchi ili kuisaidia serekali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa urahisi.

Wakipokea vifaa hivyo baadhi ya masheha na watendaji wa shirika hilo wamesema kabla ya kupewa vifaa hivyo wamekuwa wakitembea masafa marefu kwa kutumia usafiri wa kienyeji jambo ambalo limekuwa likiwaathiri katika utendaji wao huku wakisema kukabidhiwa vifaa hivyo kumekuja wakati muwafaka ambapo vitakwenda kuwaondolea changamoto hizo.

Sauti ya Bi Edtha Turuka

Vifaa vilivyotolewa kwa watendaji hao ni pamoja na Magari, Bajaji na Vishikwambi.