Tumbatu FM
Tumbatu FM
11 January 2026, 11:23 am

“Kukosekana kwa taaluma kabla ya kuingia kwenye ndoa hasa kwa vijana wa sasa hupelekea migogoro na kuongezeka kwa wimbi la talaka”
Na Vuai Juma
Viongozi wa dini wametakiwa kuwahimiza wanajamii kujifunza elimu ya ndoa ili kujiepusha na migogoro ndani ya familia.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa jumuiya ya Nataraji Social Devlopment Foundation Sidik Juma Khamis wakati akizungumza na maimamu pamoja na walimu wa madrasa katika mwendelezo wa mafunzo ya elimu ya ndoa yaliyofanyika katika tawi la skuli ya Vivid Dream Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema lengo kubwa la kuwapa elimu viongozi hao ni kuitengeneza jamii katika mfumo mzima wa maisha ya ndoa kwani kumekuwa na matatizo mengi ambayo yanawakumba wanandoa kwa kuikosa elimu hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo ukhut Namboto Khamis Juma amesema ipo haja ya kuendelea kutolewa mafunzo hayo kwa vijana kutokana matatizo yaliyomo kwenye ndoa ambayo yanasababishwa na mporomoko wa maadili.