Tumbatu FM
Tumbatu FM
21 October 2025, 8:08 am

“Kufuatia matokeo hayo wamiliki wa vyombo vya habari wanahitaji kuongeza juhudi zaidi katika kufikia mkakati wa serikali unaolenga kuwa na 50% ya uwakilishi sawa kwenye vyombo vya maamuzi ikiwemo Bunge na Baraza la wawakilishi kwa upande wa Zanzibar kwa kuruhusu mgawanyo wa madaraka wenye kuzingatia usawa kwenye vyombo vyao na kutoa fursa sawa kwenye ushiriki wa vyazo vya vipindi wakati wa kutaarisha vipindi“
Na Juma Haji Tumbatu FM
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Dr Rose Ruben amesema dhamira ya kuazisha madawati ya jinsia kwenye vyombo vya habari Nchini ni kuongeza kasi ya kufikisha dhana ya usawa wa kijisia mjini na vijijini.
Akifungua majadiliano ya kutafuta namna bora ya utekelezaji wa sera ya jinsia kwa vyombo vya habari katika hotel ya Seashells jijini Dar es salam amesema maamuzi ya TAMWA ya kuazisha madawati ya kuripoti habari za jinsia kwenye vyombo vya habari yamelenga kuwaongezea uelewa waandishi wa habari juu ya masuala ya jinsia juu ya namna yanavyohitaji kuripotiwa kutoka kwenye jamii na kuleta mafanikio makubwa kwenye Nchi.
Akitaja moja kati ya matokeo mazuri na ya kupigiwa mfano kwa Tanzania tokea Tamwa kuanza utetezi wa masuala ya jinsia amesema ni pamoja na kusikika kwa sauti za makundi ya kijamii kwenye vyombo vya habari na ongezeko la muingiliano kati ya wanawake na wanaume katika sehemu za kazi .
Wakiwasilisha maada kwenye majadiliano hayo, muhadhiri msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Dr Zuhura Khatibu na Mwalimu Rose Haji Mwalimu ambaye ni mkufunzi wa maswala ya jinsia Tanzania wamesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa kupinga vitendo vya udhalilishaji Tanzania “TGNP” mwaka 2020 unaonesha kuwa bado waandishi wa habari nchini wanakabiliwa na changamoto ya ushiriki mdogo wa fursa sawa kwenye uongozi “mgawanyo wa madaraka katika vyobmo vya habari”
wamesema kufuatia matokeo hayo wamiliki wa vyombo vya habari wanahitaji kuongeza juhudi zaidi katika kufikia mkakati wa serikali unaolenga kuwa na 50% ya uwakilishi sawa kwenye vyombo vya maamuzi ikiwemo Bunge na Baraza la wawakilishi kwa upande wa Zanzibar kwa kuruhusu mgawanyo wa madaraka wenye kuzingatia usawa kwenye vyombo vyao na kutoa fursa sawa kwenye ushiriki wa vyazo vya vipindi wakati wa kutaarisha vipindi
“Huko tuliotembelea tumekuta malalamiko mengi, waandishi wanalalamika na wengine imebidi waache kazi”. amesema Mwalimu Rose Haji Mwalim
Wakichangia kwenye majadiliano hayo baadhi ya waandishi walioshiriki Joseph Sabinus kutoka Garzeti la habari leo Na Zania Miraji kutoka Dodoma FM wamesema chazo kikuu ni kutotekelezeka vyema kwa sera ya jinsia kwenye vyombo vya habari ni kutokuwepo na machapisho ya sera ya jinsia kwenye vyombo vya habari ambayo yangeweza kuwa msaada kwa mwandishi kuzingatia kwenye kazi zake.
Majadiliano ya kujadili namna ya kuboresha utekelezaji bora wa sera ya jinsia ni sehemu ya mpango malum wa kutekeleza sera ya kijinsia kwenye vyombo vya habari unaotekelezwa na Tamwa Tanzania, Shirika la IMS na MCT. kutoka mwezi june na unategemewa kukamilika mnamo mwezi novemer 2025