Tumbatu FM
Tumbatu FM
3 August 2025, 2:34 pm

“Tuwahutubie waumini wa dini ya kiislam kuhusu hijja kumekuwa na mabadiliko kwa wale wanaotaka kwenda Makka wanatakiwa kujiandikisha mapema huu ni utaratibu uliowekwa na uongozi wa Makaa”
Na Juma Haji Juma
Mashekh na maimamu Nchini wametakiwa kutoa khotba ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kujisajili mapema kwa wananchi wenye nia ya kushiriki ibada ya hija mwaka 1447 hijria.
Akielezea utaratibu wa ibada ya hijja ya mwaka 2025 sawa na mwaka 1447 hijiria kwa wananchi wa Tumbatu katika hafla ya kutoa Elimu juu ya umuhimu ya kuhifadhi historia ya kiislam Mkurugenzi wa Wakfu Amana na Hijja kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Hajjat, Madina Haji Khamis amesema utaratibu uliozoweleka wa kutoa hotba za hija kwenye miskiti katika mwezi wa ramadhani hautosaidia kufikisha elimu kwa wakati.
Hajjat, Madina amesema kuwa kutokana na ongezeko la watu wenye uhitaji ya ibada ya hijja Nchi ya makka imeweka ukomo wa kupokea majina ya mahujjaji mwezi 20 shaaban kwa hija ya mwaka huu na yoyote atakaejitokeza kuomba nafasi ya kuhiji atapangiwa mwaka unaofuata.
Aidha amesema katika kuhakikisha kila mwananchi anapata uwezo wa kuhiji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar imeazisha mfuko wa hijja ambao utamuwezesha mwananchi mwenye kipato cha chini kuweka akiba kwa ajili ya mataarisho ya safari ya hijja.
Akizungumzia swala la kuweka wakfu wa mali Shekh Mohamed Ali Mohamed kutoka Kamisheni ya Wakfu amesema ili kuepusha waislamu kuwa omba omba ni lazima watu wenye uwezo kuweka mali zao wakfu ili zisaidie uendeshaji wa shughuli za uislamu.
Aidha Shekh Mohamed amewataka waislam wa sasa kuwaiga wasilam waliopita ambao waliekeza nguvu na mali zao kusaidia huduma za miskiti, madrasa na kutoa misaada kwa mayatima na watu wasiojiweza.
Wakitoa shukuran baadhi ya washiriki wa hafla hiyo Mw Juma Omar Juma, Mw Jecha Ali Saleh na wananchi wa Tumbatu kwa ujumla wameishukuru Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana kuwapatia elimu na kuwataka kuendeleza utamaduni huo wa kutembelea waislam.
Ziara ya hiyo ilihusu kuhamasisha wananchi kuhifadhi nyaraka Pamoja na Mejngo ya historia ya kisiwani Tumbatu sambamba na kutembelea mjengo ya historia yaliyopo eneo la Makutani pamoja na kutoa Sadaka ya misahafu, Chaki Pamoja na Nguo kwa watoto wa Tumbatu.