Tumbatu FM
Tumbatu FM
1 July 2025, 11:04 am

“Ili kufikia dhamira ya uchumi wa bluu lazima tutunze mazingira kwenye bahari kwa kuepuka kuharibu mazalia ya Samaki”
Na Vuai Juma
Wananchi wametakiwa kulinda na kutunza rasilimali za bahari ili kuendeleza dhana ya uchumi wa buluu kama ilivyo azma ya serikali ya kuajiri watu wengi ndani ya sekta ya uvuvi.
Kauli hiyo imetolewa na Ndugu Ali Makame kutoka idara ya maendeleo ya uvuvi na mazao ya baharini wakati akizungumza na wakazi wa mkoa wa kaskazini unguja kwenye kipindi maalum kuhusu sualazima la utunzaji wa mazingira ambacho kimerushwa kupitia kituo cha radio jamii Tumbatu.
Amesema ili jamii iweze kupata maendeleo kupitia kazi ya uvuvi ni lazima kuwe na utaratibu wa kuhifadhi mazingira katika maeneo ya Bahari.
Hata hivyo amesema serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbali mbali katika kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira Baharini lakini bado kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya watu kutofika maeneo ya kutoa elimu hiyo jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa uharibifu wa rasilimali za Bahari huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa kutolewa kwa taaluma inayohusu masuala ya Bahari.
Kwaupande wake Shehe Awesu Shehe Afisa miradi wa jumuiya ya Jongowe Developmenti Foundation amesema sekta ya uvuvi inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na uvuvi haramu mambo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kuathiri mazingira na viumbe wa baharini.