Tumbatu FM
Tumbatu FM
1 July 2025, 10:00 am

“Viongozi wote wanawajibu wa kutoa taari ili wananchi waweze kuzifaham na kujua kinacho endelea”
Na Vuai Juma.
Watendaji wa sekta za kiserikali ndani ya mkoa wa Kaskazini Unguja wametakiwa kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utendaji wao ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi.
Akizungumza na wandishi wa Habari huko ofisini kwake Mkokotoni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Matar Zahoro Masoud amesema viongozi wote wanawajibu wa kueleza tarifa kwa wandishi wa Habari ili waweze kuwafikishia wananchi walio chini hasa maeneo ya vijijini.
Amesema tayari amekwisha toa maagizo kwa wakuu waote wa taasisi zilizo chini yake kuhakikisha wanatoa tarifafa ambazo wanajamii wanapaswa kuzifaham hali itakayopelekea kutanua wigo wa mawasiliano kati ya serikali na watu wake.
Hata hivyo amewataka wandishi wa Habari kujiepusha na utowaji taarifa ambazo zitaleta taharuki katika jamii ili taifa liweze kubaki salama na kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.