Tumbatu FM
Tumbatu FM
25 June 2025, 11:49 am

Pichani ni walimu pamoja na wanafunzi wa skuli ya sekondari Tumbatu wakiwa na wajumbe wa (WOMESA) Tanzania.
Picha na Vuai Juma.
Mabadiliko kwa sasa ni lazima ili tuweze kufanya kazi ya ubaharia kwa weledi vijana ni lazima msome kwa bidii ili kuleta mabadiliko ya kitaalamu.

“Ni Picha ya mwenyekiti wa maadhimisho ya siku ya ubaharia duniani upande wa Tanzania Stela katondo (aliye simama)”
Na Vuai Juma.
Umoja wa wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya Bahari ukanda wa Afrika mashariki na kusini tawi la Tanzania umewataka wanafunzi wa kike wa skuli ya sekondari Tumbatu kuchagua fani ya ubaharia wakati wanapojiunga katika elimu ya ngazi ya vyuo kutokana na faida zilizomo ndani ya kada hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa maadhimisho ya siku ya ubaharia duniani upande wa Tanzania Stela Katondo wakati akizungumza kwenye mkutano maalum wa kutoa elimu kuhusu taaluma ya ubaharia uliowakutanisha wanachama wa WOMESA ofisi za Tanzania walimu Pamoja na wanafunzi wa skuli hiyo.
Amaesema nilazima wajamii iwathamini na kuwaenzi mabahari kutokana na mchango wao huku akikemea utendaji wa kazi hiyo kwa mazowea yaliyopo ya kuendesha vyombo vya baharini kwa kwa mifumo ya kizamani badalayake waisome kazi hiyo na kuilewa ili waweze kutunza mazingira na kujiepusha na athari zinazoweza kujitokeza.
“Tunatakiwa tuache mazowea ya wazee wetu wa nyuma ambao huendesha vyombo vya usafiri wa baharini kimazowea jambo hili ni hatari sana katika maisha yetu chamsingi ni kusoma fani ya ubaharia imekushanya mambo mengi tutapata fursa nyingi pia”

Ni afisa masoko mawasiliano kutoka WOMESA Tanzania Farida Shaban ( aliyessimama na kushika kipeperushi)
Picha na Vuai Juma.
Kwaupande wake afisa masoko na mawasiliano kutoka umoja huo Farida Shaban Zoange amesema niwakati wa wanawake kujiingiza kwa wingi katika sekta hiyo kutokana na uwezo walionao wanawake kwenye Nyanja hiyo.
Aidha amewataka kusoma masomo ya sayansi kwa bidii Pamoja na kujiamini jambo ambalo litawawezesha kuondokana na usumbufu wanaposoma ubaharia na kupelekea kuifaham vizuri fani hiyo.
“Dunia ya sasa ni ya mabadiliko wanawake tunaweza kufanya kazi nyingi tusiogope tujiamini hakika tunaweza ” ni kauli ya Farida.


Picha ni Mwalim Juma Gora na Mwanafunzi Subira makame kutoka skuli ya sekondari Tumbatu.
Picha na Vuai Juma.
Kwaupande wao mwalim Juma Gora na mwanafunzi Subira Makame Wakizungumza kwa niaba ya Skuli ya Tumbatu wamesema wanawashukuru wanawake mabaharia kwa kuamua kuwapatia elimu hiyo huku wakiwaomba kuendelea na utaratibu huo kila mwaka kwani wamepata kujifunza mambo mbali mbali.
“Tumepokea kwa mikono miwili elimumhii na tunatoa pongezi zetu zote kwenu tunaomba muje kwa mara nyengine mutupe muendelezo huu”
Maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 25 June ya kila mwaka.