Tumbatu FM

Mwenge wa uhuru wan’gara Kaskazini ‘A’ kwenye miradi ya maendeleo

20 June 2025, 4:59 pm

Picha ya wakitembeza mwenge wa uhuru kwenye eneo la mradi wa hoteli ya kappa sense iliyopo pwani mchangani Wilaya ya kaskazini “A” Unguja.

Picha na Juma Haji Juma.

Naagiza “taarifa zote za miradi zitunzwe ili ziweze kutumika baada ya mbio hizi za mwenge kwa ajili ya maendeleo ya miradi hiyo”

Na Juma Haji Juma.

Mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2025 zimeendelea katika Wilaya ya kaskazini “A”Unguja na kuzindua miradi mbali mbali ndani ya Wilaya hiyo.

Mbio hizo zilitanguliwa na Makabidhiano ya mwenge wa uhuru yaliyofanyika mapema katika uwanja wa mpira  wa upenja JKU ambapo Mkuu wa Wilaya ya kaskazini “a ” Mhe Rashidi Simai Msaraka alipokea mwenge huo pamoja na zana zote  zilizotaarishwa kutumika kwenye matembezi.

Awali kiongozi wa mwenge wa uhuru mwaka 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi akitoa nasaha zake wakati wa mapokezi ya mwenge ameagiza viongozi wa miradi yote iliyotembelewa na mwenge kuhakikisha kuwa taarifa za miradi zinawekwa pamoja ili jamii ijufunze baada ya kukamilika kwa matembezi ya mwenge.

Baadhi ya maeneo yaliyopitiwa na mwenge ni pamoja na bonde la mpunga kinyasini, Mradi wa mahakama ya Wilaya ya Kaskazini “a” iliopo Mkwajumu , ufungazi wa mafunzo ya uchaguzi yaliyofanyika katika baraza la manispa la Wilaya ya kaskazini “A”, ujenzi wa skuli ya msingi Potoa, ukaguaji wa zoezi la uchunguuzi wa afya pamoja na maonesho ya wajasiriamali wa kijiji cha Nungwi.