Tumbatu FM
Tumbatu FM
16 June 2025, 5:37 pm

Picha ya Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja akiwa na wandishi wa habari kwenye kikao cha kutoa tarifa juu ya ujio wa mwenge wa uhuru Kaskazini Unguja.
Picha na Vuai Juma
“Miradi ambayo inapitiwa na Mwenge wa uhuru ni alama ya ya ukuaji wa maendeleo katika nchi yetu”
Na Vuai Juma
Serikali ya mkoa wa kaskazini Unguja imesema ujio wa Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu kutapelekea kuiunua mkoa huo katika sekta ya kimaendeleo.
Akizungumza na wandishi wa Habari katika ofisi zake zilizopo Mkuu wa Mkoa huo Matar Zahoro Masoud amesema Mwenge wa uhuru ni alama muhimu ya taifa ambayo inapaswa kutunzwa na kuenziwa kwa maslahi ya taifa.
Amesema mwenge huo utapitia miradi saba ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali ambapo miradi minne itawekewa mawe ya msingi miradi miwili itatembelewa na ufunguzi wa mradi mmoja.
Hata hivyo amesema miradai hiyo ambayo imejumuisha miradi ya watu binafsi itagharimu jumla ya shilingi bilioni 123 huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na maeneo Jirani kutoa mashirikiano katika kuupokea Mwenge huo huku akisema kukamilika kwa miradi hiyo itakwenda kuwanufaishi wananchi.
Mwenge wa uhuru utawasili ndani ya mkoa wa kasakazini unguja siku ya tarehe 19 mwezi huu na utatembezwa kwa muda wa siku mbili katika wilaya zote za mkoa huo ambapo Kauli mbiu ni Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.