Tumbatu FM

NAPAC na UNDP Waja na Msaada wa Kisheria Kupambana na Ukatili na Migogoro ya Kijamii

16 June 2025, 10:57 am

Picha ya wananchi kutoka shehia nne za mkoa wa Kasakazini unguja wakiwa katika mkutano wa pamoja na wanajumuiya ya Napac.

Picha na Abdul-Sakaza

“Msada wa kisheria kwa wanajamii utasaidia kupatikana kwa haki na kutatua vitendo vya udhalilishaji kwa wananchi”

“Picha ya mkurugenzi wa jumuiya ya Napac Asia Fadhil Makame”

Na Abdul – Sakaza

Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Kaskazini A (NAPAC) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) imezindua huduma ya msaada wa kisheria kwa wakazi wa shehia nne za Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la utoaji wa elimu hapo jana shehia ya muwanda , Mkurugenzi wa NAPAC, Bi. Asia Fadhil Makame, alisema kuwa msaada huo unalenga kutoa elimu ya kisheria na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ya kila siku.

“Tunatambua kuwa migogoro mingi ya kijamii, ukatili wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za binadamu vinasababishwa na wananchi kutojua haki zao. Ndiyo maana tumeamua kupeleka huduma hii hadi vijijini,” alisema Bi. Asia.

Sauti ya bi Asia Fadhil ambaye ni mkurugenzi wa jumuiya ya Napac iliyopo Kaskazini Unguja

Aidha, alibainisha kuwa huduma hiyo si tu kusikiliza malalamiko, bali pia kutoa ushauri na njia sahihi za kufuata ili kutatua migogoro kwa mujibu wa sheria.

“Picha ua mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Kaskazini Unguja Salum Khamis Machano”

Picha Na Abdul – Sakaza

Tunahitaji mashirikiano ya karibu kati ya jamii na vyombo vya ulinzi na usalama. Dawati la Jinsia liko tayari kushirikiana na mashirika kama NAPAC ili kuhakikisha vitendo vya ukatili vinaisha

Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Kaskazini Unguja, Inspecta Salum Khamis Machano, alisema jitihada za NAPAC zinapaswa kuungwa mkono na jamii nzima kwa kuwa zinagusa maisha ya watu moja kwa moja.

Sauti ya Mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Picha ya mkazi a kijiji cha muwanda bwana Haji Machano Makame akizungumza kwenye kikao cha wananchi na jumuiya ya Napac

“Tunaishukuru NAPAC kwa kutufikia huku vijijini ,Tumeelimika na sasa tunaweza kutetea haki zetu bila woga,” alisema mkazi mmoja

Kwaupande wake bwana Haji Machano Makame akizungumza kwa niaba ya wanashehia wezake amesema wamefurahishwa na ujio wa ambayo itawasaidia kupata maarifa yatakayowasaidia kupambana na changamoto wanazokutana nazo.

Ni sauti ya mkazi wa shehia ya muwanda bwana Haji Machano Haji.

Huduma hiyo inayotolewa kupitia mradi wa LEAP II (Legal Empowerment and Access to Justice Program), inalenga kuwafikia wakazi wa Kigongoni, Mkokotoni, Muwanda na Tumbatu Jongowe, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha haki na usawa vinapatikana kwa kila mmoja.