Tumbatu FM

Wizara ya elimu Zanzibar kuongeza wataalamu wa fani mbali mbali

11 June 2025, 5:02 pm

Picha ya waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Lela Muhamed Mussa.

Picha na Vuai Juma.

Kuwepo kwa walimu ambao ni wabobevu kwenye wlfani tofauti hapa Zanzibar ikiwemo sekta ya anga kutawawezesha wanafunzi kupiga hatua katika eneo hilo“.

Na Vuai Juma.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa amesema Serikali inaendelea kuleta wataalamu na wabobezi wa fani mbalim bali za masomo ya kisasa ili kujenga taifa lenye wasomi na wabunifu.

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kuwajengea uwezo wanafunzi wa Sekta ya Anga katika Uwanja wa Hanga la Anga Chuo cha Taasisi ya Sayansi ya Karume amesema Serikali imeleta fani za kisasa zinazohitajika duniani, ndani ya Zanzibar na katika Taasisi ya Karume.

Amesema kuwa ni fursa muhimu kwa wanafunzi wa fani hiyo ambayo itawawezesha wanafunzi hao kwenda kujifunza katika mataifa mbali mbali Duniani ili kuitangaza Zanzibar.

Aidha ameeleza kuwa kuwepo kwa mkutano huo ni hatua nzuri ya kuifungua Zanzibar na kukitangaza Taasisi ya Karume na Programu wanazozitoa ili kuweza kupata wanafunzi wengi kutoka nchi mbalimbali duniani.

Amefafanua kuwa hatua hiyo inaonesha umahiri wa fani zinazosomeshwa ndani ya Zanzibar zina ubora na ushindani katika dunia.

Hata hivyo amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya upatikanaji wa fursa za fani ya teknolojia pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Nae Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume Dkt. Mahmoud Adulwahab Al-lawi amesema kupitia mkutano huo wanatarajia kutengeneza fursa mbalimbali kwa wanafunzi wa fani ya anga kupitia Kampuni za Anga ili kuwajengea uzoefu na kupata nafasi za ajira kupitia Kampuni hizo.

Aidha amefafanua kuwa ujio wa Makampuni hayo ya Anga utasaidia kuendeleza fani ya anga na kufungua milango ya kuongeza ujuzi na utaalamu walimu na wanafunzi na kupata mbinu na vifaa vipya kwa ajili ya mafunzo ya fani hiyo.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Ushauri katika Kampuni ya Aviadev Afrika, Sean Mendis ameahidi kuendeleza ushirikiano katika kuimarisha Sekta ya Anga Zanzibar pamoja na kuwaunga mkono wanafunzi wa fani hiyo ili kufikia malengo.