Tumbatu FM
Tumbatu FM
10 May 2025, 1:13 pm

Pichani ni katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Hijji Shajak (alievaa koti jeusi) akikabidhi zawadi za tunzo ya Samia kalam award 2025 katika Ofisi ya Wizara ya Habar Zanzibar.
Picha na Abdul-Sakaza.
“Tumieni tunzo mliyopatiwa katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika kituo chenu sambamba na kuinua uwezo wa wafanyakazi kiutendaji na kielimu ili mfikishe taarifa zinazoigusa jamii kwa umakini”
Na Juma Haji
Uongozi wa Radio jamii Tumbatu umekabidhiwa zawadi zilizopatikana kwenye tunzo ya Samia award iliyotolewa katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salam.
Akikabidhi zawadi hizo mbele ya katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndugu Hijji Sajak amewataaka viongozi na wafanyakazi wa Radio Tumbatu FM kuendeleza mazuri yaliyopelekea kuipata tunzo hiyo ili kuwa na sifa za kuendelea kuaminika na kufanya kazi zenye tija kwa jamii ya Mkoa wa kaskazini Unguja.
kwa upande wake katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi Fatma Hamadi Rajab amesema wamefurahishwa na upatikanaji wa tunzo hiyo huku wakiahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kituo cha Radio Jamii Tumbatu sambamba na kuwataka wafanyakazi kuandika habari kwa kuzingatia maadili ya kazi.
Aakipokea zawadi hizo mkurugenzi wa Tumbatu FM Vuai Juma Makame ameushukuru uongozi wa Tamwa,TCRA, Wizara ya Mawasiliano Zanzibar na Wizara ya Habari Zanzibar kwa kuendelea kuwaunga mkono waandishi wa habari kwenye kazi zao.
Zawadi zilizotolewa ni pamoja na Fedha Taslim Sh 5,000,000/= na Komputa moja.