SMZ yafungua shamba jipya la uchotaji wa mchanga
3 October 2024, 8:03 am
Picha ya Waziri wa Maji, Nishati na Madini Shaibu Hassan Kaduara (alievalia shati jeusi) akiwa katika kikao na wandishi wa habari kuhusu ufunguzi wa eneo jipya la uchotaji wa mchanga.
Na Latifa Ali.
“Nivyema kuweza kufuata vifaa vya ujenzi kama mchanga na kokoto katika maeneo yaliotengwa na serekali”.
Na Latifa Ali.
Wizara ya Maji, Nishati na Madini imelifungua shamba la ndugu Othman Khamis Ame liliopo Donge Mchangani Wilaya ya Kaskazini A Unguja kwa ajili ya kutoa huduma mbali mbali za miradi ya ujenzi.
Taarifa hiyo imetolewa mbele ya wandishi wa habari na waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaibu Hassan Kaduara katika ukumbi wa Wizara hiyo uliopo Maisara mjini zanzibar.
Amesema wizara inatoa taarifa hiyo kwa wananchi kuwa imelifungua shamba hilo baada ya lile la zamani la Ndugu Azizi Khamis Azizi liliopo Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini A Unguja kumalizika kwa mchanga unaofaa kwenye bonde hilo ambao ulikua unatumiwa kwa shughuli za ujenzi huku akitoa onyo kwa baadhi ya madereva kusingizia ugumu wa upatikanaji wa vibali na kuwalangua wananchi.
Amefahamisha kuwa Serikali inaendelea kuzuia matumizi na usafirishaji wa mawe katika shughuli za ujenzi na kuvitaka viwanda vinavyojishughulisha na uzalishaji wa kokoto kufanya shughuli zake katika maeneo yenye mawe ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha amewashauri wananchi kubadilisha utamaduni wa ujenzi na kutumia tofali badala ya mawe kama ilivyo katika mikoa mengine ya Tanzania bara.