Tumbatu FM

Kikobweni yakabiliwa na changamoto mbalimbali

2 October 2024, 10:15 am

Picha ya Mbunge wa Jimbo la Donge Juma Usonge (aliyevaa koti jeusi na kofia) akiwa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi wa shehia ya Kikobweni.

Na Latifa Ali.

“Viongozi wanapaswa kuwa mstari wa mbele kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao ili waondokane na athari katika jamii”.

Na Latifa Ali.

Wanakijiji wa shehia ya Kikobweni jimbo la Chaani wilaya ya Kaskazini A Unguja wamelalamikia juu ya uwepo wa changamoto mbalimbali katika shehia yao.

Hayo yamebainika katika kikao maalum cha kusikiliza matatizo yaliyopo kwenye eneo hilo kilichoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo ndugu Juma Usonge huko uwanja wa mpira wa Kikobweni mkoa wa Kaskazini Unguja.

Wamesema kwa sasa wanakabaliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama, wizi uliokithiri, kugeuzwa eneo la kituo cha afya cha Kikobweni kama sehemu ya kufanyiwa vitendo viovu pamoja na uchakavu wa kituo hicho.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo amekiri kupokea taarifa za uwepo wa matatizo hayo kutoka kwa uongozi wa shehia huku akiahidi kuyafanyia kazi ili kuleta utulivu kwa wananchi wake .