Tumbatu FM

CCM Kaskazini Unguja yaridhishwa na utekelezaji wa miradi

5 July 2024, 4:32 pm

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndugu Iddi Ali Ame akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha na AbdulSakaza.

Kukamilika kwa miradi ya kimkakati katika maeneo mbalimbali kutawasaidia wananchi kupata maendeleo.

Na Vuai Juma.

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja imesema imeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilinayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Iddi Ali Ame katika ziara maalumu ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi inayo tekelezwa.

Amesema halmashauri kuu ya ccm mkoa wa kaskazini unguja imeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya chama hicho inayofanywa na serikali ya Dokta Hussein Ali Mwinyi kwani miradi hiyo imelenga kutatua matatizo ya wananchi.

Picha na Vuai Juma.

Picha ya mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja (aliyevaa miwani na kofia) wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi.

Kwaupande eake Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mh.Rashid Hdid Rashid amekishukuru Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuitembelea miradi ya maendeleo ambayo imejengwa na serikali kwa kushirkiana na waekezaji na kusema changamoto zilizobainika katika miradi hiyo serekali itachukua hatua ya kuzitatua kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Jumla ya miradi saba imetembelewa ikiwemo Mradi wa Bohari ya Gesi(Oryx),Mangapwani ,Bohari ya Mafuta Mangapwani, Tangi la Maji Bumbwini, uandaaji wa vitalu vya ujenzi wa misingi na uchimbaji wa visima kibokwa,Mradi wa Hoteli ya Nyota Tano Pwani Mchangani, Soko la Mkwajuni pamoja na Skuli ya Ghorofa .