Masheha zibeni njia zinazoeneza matendo maovu
14 June 2024, 12:30 pm
Kudhibiti maeneo hatarishi kutapunguza kuenea kwa matukio ya udhalilishaji wa kijinsia.
Na Vuai Juma.
Masheha wa Wilaya ya Kati wametakiwa kuwatafuta wamiliki wa maboma na nyumba za kukodisha katika Shehia zao ili kuziba mianya ya vitendo viovu katika jamii .
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abasi Ali ametoa wito huo Dunga Wilaya ya Kati wakati alipokuwa akizungumza na masheha hao pamoja na kujadili mbinu mbalimbali zitakazoweza kuondosha matendo hayo.
Amesema kuwa yapo majengo ambayo yamekuwa yakitumika kufanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye maeneo hayo ambavyo vinasababisha athari katika jamii.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa pamoja na Waratibu wa jinsia katika shehia zao ili kuweze kukomeshwa kwa kadhia hiyo inayowakumba wanawake na watoto.
Kwa uapande wake Katibu wa Masheha wa Wilaya ya Kati Zidi Suleiman amesema watahakikisha wanaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Waratibu hao licha ya kazi ngumu wanayoifanya usiku na mchana.