Ruangwa FM

Tari yawapiga msasa maafisa ugani Lindi matumizi ya viuatilifu

13 June 2025, 5:37 pm

Na Khadja Omari

Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tanzania Kituo cha ( TARI NALIENDELE) imetoa Mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viwatilifu vya zao la korosho kwa maafisa Ugani wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

Mafunzo hayo yamefanyika Katika Mashamba ya Jkt huko Ngongo Manispaa Lindi yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo Maafisa ugani watakaokaenda kuwafundisha Wakulima hasa kipindi hiki ambacho wamepatiwa pembejeo

Mtafuti uhalishaji wa teknolojia, tari naliendele Gasper Mgimiloko amesema kupitia Mafunzo hayo wanalenga kuwafikia maafisa ugani 336 kwa mkoa mzima wa lindi kati yao 152 ni wa program maalum ya BBT

Kwa upande wake Mtafiti wa Kilimo Tari Naliendele William Mbasa amesema mafunzo hayo yamejikita kwenye sehemu ya utambuzi wa visumbufu, namna ya kuvidhibiti na matumizi ya mashine ya kupulizia viwatilifu sambamba na magonjwa ya mikorosho

Nao maafisa kilimo wamesema mfunzo hayo watakwenda kuwafanya wakulima waweze kuzalisha kwa tija ili wapae mazao bora Zaidi kwani kulikua na changamoto haswa za mabadiliko ya tabia ya nchi