Kahama FM

Polio yabisha hodi Mwanza, Kahama yazindua utoaji chanjo

March 25, 2026, 4:25 pm

Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa  Kahama Dkt. Herry Sylivester akizindua chanjo ya polio katika Manispaa ya Kahama

Na Sebastian Mnakaya

Watoto takribani 145,820 wanatarajiwa kufikiwa na chanjo ya  polio  Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga huku watoa huduma ya chanjo wakitarajia kuwafikia watoto hao nyumba kwa nyumba, stend, sokoni, shule, vituo vya kulea watoto na  kliniki.

Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa  Kahama Dkt. Herry  Sylivester amesema  hayo leo kwenye uzinduzi wa utoaji wa chanjo huku akieleza watoto wanao takiwa kupata chanjo ni wenye umri chini ya miaka kumi.

Dkt. Sylivester amesema uhamasishaji umefanyika kwa njia mbalimbali ili kuweza kuwafikia walengwa kupata chango ya polio, huku akisema mtoto asipopata chanjo hiyo na akipata ugonjwa wa polio unaweza kumsababishia ulemavu wa kudumu wakati mwingine kifo.

Sauti ya Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa Kahama Dkt Herry  Sylivester

Kwa upande wao, baadhi ya wazazi ambayo watoto wao wamepatiwa chanjo hiyo akiwemo Rehema Mngaya na Christina Lucas wameishukuru serikali kwa kutoa chanjo hiyo ambayo itawasaidia watoto wao wasipate magonjwa wa polio.

Sauti za wazazi Rehema Mngaya na Christina Lucas

Vimelea vya ugonjwa wa polio vimebainika mkoani Mwanza kwenye majitaka  na hivyo serikali kuchukua jukumu la utoaji wa chanjo kwa  mikoa saba ya Kanda ya Ziwa ikiwa hapa nchini Tanzania mgonjwa wa polio mara ya mwisho alibainika mwaka 1996.