Kahama FM

Wananchi Kahama watakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji

August 20, 2025, 5:32 pm

mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS Prof Faustine Kamuzora (Picha na Sebastian Mnakaya)

Wananchi wilayani Kahama changamkieni fursa za uwekezaji na kampuni ya Uwekezaji ya UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS)

Na Sebastian Mnakaya

Wananchi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia fursa ya kuwekeza fedha zao na kampuni ya ya Uwekezaji ya UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS) ili waweze kupata maendeleo katika sekta mbalimbali.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho ambapo amesema ufunguzi wa tawi hilo ni kielelezo cha dhamira ya UTT AMIS kupanua huduma zake na kuwawezesha wananchi kupata elimu ya fedha, akiba na uwekezaji kwa urahisi zaidi.

Nkunda amewataka wananchi wa Kahama na maeneo mengine kwa ujumla kutumia ipasavyo fursa zinazotolewa kituo hicho itasaidia kupata mitaji katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji na biashara.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda

Aidha Nkinda amesema kuwa ujio wa kituo hicho katika wilaya ya kahama itaongeza mafanikio makubwa kwa haraka zaidi, huku serikali ikiendelea kuboresha sera za uwekezaji nchini.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS Prof Faustine Kamuzora

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS Prof Faustine Kamuzora, amesema kuwa wilaya ya Kahama imekuwa ikikukuwa kiuchumi kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uchimbaji wa madini, kilimo na biashara hali iliyosbabisha kuweka tawi la UTT AMIS Kahama.

Sauti ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT AMIS Prof Faustine Kamuzora
Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS Simon Migangala

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS Simon Migangala amesema tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo imendelea kukua na kuwa na wawekezaji wengi, huku akiishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS Simon Migangala

Tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo imesimamia rasilimali zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 3.5, huku ikihudumia karibu wawekezaji 500,000 kupitia mifuko mbalimbali inayotoa faida ya wastani wa asilimia 12–15 kwa mwaka kulingana na mwenendo wa soko.