Kahama FM
Kahama FM
May 31, 2025, 3:34 pm

Waaguzi katika Manispaa ya Kahama wamepewe motisha kutokana na kazi ngumu na hatarishi wanayofanya
Na Sebastian Mnakaya
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya kahama Masudi Kibetu kutoa motisha kwa wauguzi wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi ikiwemo kuwahudumia wenye magonjwa ya kuambukiza.
Mboni ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika mahadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambapo kwa wilaya ya Kahama yamefanyika katika kituo cha afya Nyasubi kilichopo Manispaa ya Kahama, .
Aidha, Mhita ameiomba halmashauri ya Manispaa ya Kahama kutenga bajeti kwa ajili ya wauguzi hao kupata mafunzo mbali mbalimbali yanayohusu taaluma yao, ikiwemo mikutano na makongamano, huku Manispaa hiyo ikitakiwa kuendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na nyumba za watumishi.

Awali akisoma risala ya Katibu wa Chama cha Wauguzi Manispaa ya Kahama Agnes Mkanga amesema kuwa wauguzi hawapewi motisha ya mazingira hatarishi licha ya kuwahudumia wagonjwa wa kifua kikuu,homa ya ini na magonjwa mengine ya kuambukiza.
Siku ya wauguzi duniani huadhimishwa kila ifikapo May 12 ya kila mwaka, Na kwa mwaka 2025 kauli mbiu ni “Uuguzi Nguvu ya Mabadiliko”
